Niwonapo Mti Bora
Tenzi za rohoni ( #84 ) , Nyimbo standard ( #169 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Niwonapo mti bora, Kristo aliponifia, kwangu pato ni hasara, kiburi nakichukia.
Na nisijivune, Bwana, ila kwa mauti yako; upuzi sitaki tena, ni chini ya damu yako.
Tangu kichwa hata nyayo, zamwagwa pendo na hamu, ndako pweke hamu hiyo, pendo zako zimetimia.
Vitu vyote vya dunia, si sadaka ya kutosha; pendo zako zinawia nafsi, mali, na maisha.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook