Natoka Leo Mbinguni
Lyrics kama ilivyo katika "Mwimbieni Bwana (Tumwabudu Mungu wetu)"
Natoka leo Mbinguni,
naleta habari njema
Habari yenye furaha
kwa ninyi na watu wote.
Amezaliwa kitoto,
na mwana mwali maria,
ni mtoto mzuri na
mwema, awaletea furaha.
Ni Yesu,
Mwana wa Mungu,
Mwokozi wa ulimwengu,
Atakayekuondoa
makosa yote na shida.
Awapa wote wokovu,
uliowekwa na Mungu,
mkae nanyi mbinguni
pamoja nasi milele.
Alama yenu iwe hii:
Zizini mtoto maskini
aliyevikwa viguo,
naye ni Bwana wa mbingu.
Tumsifuni sisi sote,
tuwafuate wachunga,
tuyaone yale makuu,
tuliyopewa ma Mungu.
Yesu unipendezaye,
ugeuze moyo wangu,
uwe nyumba yako nzuri,
nisikuache daima.
Tumsifu Bwana wa
mbingu,
aliyemtoa mwanawe.
Twumwimbie kwa furaha,
pamoja nao malaika.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook