Akifa Yesu nikifa naye
Tenzi za rohoni ( #18 ) , Nyimbo standard ( #354 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Akifa Yesu nikafa naye; uzima upya huishi naye; humtazama mpaka aje; nyakati zote ni wake yeye.
Nyakati zote nimo pendoni, nyakati zote ni uzimani, humtazama hata atokee, nyakati zote mimi ni wake.
Vita sipigi visivyo haki, na Bwana wangu hapiganiki; beramu yake haitwaliki, napo po pote hila sitaki.
Sina mashaka, akawa mbali; mizigo yote ahimili; ananituliza Imanweli, nyakati zote mimi husali.
Sina huzuni na mimi sidhii; simwagi chozi, wala siguni; sikuti afa, ila kitini daima hunifikiri mimi.
Kila unyonge huusikia; kila ugonjwa kwake hupoa; Yesu ni mwenyewe kuniokoa nyakati zote hunujalia.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook