Kwa Wingi wa Nyama
Tenzi za rohoni ( #83 ) , Nyimbo standard ( #247 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Kwa wingi wa nyama, na sadaka pia, hupata wapi salama, kwondoa hatia?
Sadaka ni Yesu, Hwondoa makosa; dhabihu mwenye jina kuu, atanitakasa.
Kwa yangu imani, nikuweke sasa, mkono mwako kichwani, kukiri makosa.
Roho yakumbuka mambo ya mtini, mzigo ulijitweka, ndiyo yangu deni.
Deni hutanguka, tukimuamini; kwa damu tumeokoka, twimbe furahani.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook