Hata Ndimi Elfu
Tenzi za rohoni ( #3 ) , Nyimbo standard ( #520 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Hata ndimi elfu elfu, hazitoshi kweli, Bwana Yesu kumsifu, Kwa zake fadhili.
Yesu jina liwezalo, kufukuza hofu; Lanifurahisha hilo, Lanipa wokovu.
Jina hilo ni uzima; Ni afya; amani; Laleta habari njema; Twalipiwa deni.
Yesu huvunja mapingu, ya dhambi moyoni; Msamaha, tena nguvu, twapata rohoni.
Kwa sauti yake vile, wafu hufufuka, wakafurahi milele, pasipo mashaka.
Ewe Yesu wangu Bwana, uwezo nipewe, kuhubiri kote sana, wote wakujue.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook