Mmoja Apita Wote
Tenzi za rohoni ( #128 ) , Nyimbo standard ( #339 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Mmoja apita wote, atupenda; zaidi ya ndugu wote, atupenda; rafiki wa duniani, wote hatuwaamini; Yesu kwa kila zamani, atupenda.
Kumjua ni uzima, atupenda; jinsi ajaavyo wema atupenda; yeye ametununua, kwa damu aliyomwaga, Dhambini kutuokoa, atupenda.
Sasa tunaye rafiki, atupenda; hupenda kutubariki; atupenda; twapenda kumsikia, atwita kukaribia, nasi tutamwamania, atupenda.
Husamehe Dhambi zetu, atupenda; hushinda adui zetu, atupenda; anatwonea huruma, hatupati ila mema, anatwongoza salama, atupenda.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook