Yesu Mponya tu Hapa
Lyrics kama ilivyo katika "Mwimbieni Bwana (Tumwabudu Mungu wetu)"
Yesu mponya tu hapa,
moyo watulia,
mawazo yetu yote
uyavute kwako.
Mwanga wa Neno lako,
utuangaze wote,
tuwe na mwangazo.
Kaa karibu nasi,
tunakutamani,
mfunzi wetu na wewe
sisi wanafunzi.
Nenolo lina nguvu,
litatufanya wapya,
laongoza vema.
Tuna furaha kubwa,
tunakungojea.
Wewe u mwamba wetu
tutegemeao.
Bwana tunakushika
mpaka tunapofika
uzimani kwako.
Twataka utufunze kuwa na upole. Tufanane na wewe unyenyekeavyo. Utimizavyo kazi, ulivyofanya bidii kuwa mpatanishi.
Nguvu ya Roho wako
ionyeshe kwetu,
unavyomulika
wanaopotea.
Kwa kinywa chako Yesu
utushindie nasi,
tuwe wako kweli!


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook