Jina Moja ni Kubwa Sana
Lyrics kama ilivyo katika "Mwimbieni Bwana (Tumwabudu Mungu wetu)"
Jina moja ni kubwa sana:
Ni jina lako Bwanangu!
Nasifu jina hili lako
Yesu Kristo u Mwokozi.
Li tamu kwangu jina hili,
jina lingine silijui.
Naliandika jina hili
rohoni mwangu kabisa.
Silisahau siku zote,
halifutiki moyoni.
Li tamu kwangu Jina hili,
jina jingine sitafuti.
Jina hili ni jua langu
lawaka ndani ya roho.
Lanipa na utengemano,
lafuta makosa yote.
Li tamu kwangu jina hili,
jina lingine sifahamu.
Jina hili ni boma langu, upanga wangu vitani, ni ngao yangu na silaha, lamshinda hata Shetani. Li tamu kwangu jina hilli jina jingine siliitaki.
Jina hili lanipa nguvu,
niweze kwenda kwa haki.
Ujuzi wote umo humo
katika jina la Yesu.
Li tamu kwangu Jina hili,
jina lingine sitamani.
Ee Yesu, Jina lako ndilo furaha yangu nikifa. Ni cheti cha kuingilia mbinguni kwa Bwana Mungu. Ndipo nitalisifu sana, jina lingine silijui.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook