Ati Twonane Mtoni?
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Ati twonane mtoni? Maji mazuri ya mbingu;
Yanatokea mwangani, penye kiti cha Mungu.
Naam, twonane mtoni! Watakatifu, kwenu ni mtoni!
Tutakutanika mtoni penye kiti cha Mungu.
Tukitembea mtoni, Na Yesu mchunga wetu,
daima tu ibadani, usoni pake kwetu.
Kwang'ara sana mtoni, cha Mwokozi ni kioo,
milele hatuachani, tumsifu kwa nyimbo.
Si mbali sana mtoni, karibu tutawasili,
mara huwa furahani, na amani ya kweli.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook