Tufani Inapovuma
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Tufani inapovuma sana moyoni mwangu,
Huona pa kujificha mkononi mwa Mungu.
Hunificha, hunificha
adui hatanipata,
hunificha, hunificha, mkononi mwake.
Pengine kuna taabu yanisongeza kwake;
Naijua si hasira, ni ya mapenzi yake.
Adui wakiniudhi nami nikisumbuka,
Mungu atavigeuza vyote viwe baraka.
Niishipo duniani ni tufani daima,
anilindapo rohoni nitakaa salama.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook