Njooni Tumheshimu Yesu
Lyrics kama ilivyo katika "Mwimbieni Bwana (Tumwabudu Mungu wetu)"
Njooni, tumheshimu Yesu,
tumtolee sifa zote.
Tumwimbieni kwa furaha,
sisi watu wa Yesu
Baba amemtuma Mwana,
atuletee uzima,
utakaopewa watu,
wenye shida na kufa.
Moyo wake watupenda,
kwa uendo amekuja,
aokoe wenye dhambi,
wasishindwe na mwovu
Nuru imetutokea, Yesu akiponda kichwa cha adui wetu mkali anayetudanganya.
Tunabarikiwa kweli, tukishika Neno hili, tukimsifu Bwana Yesu kwa vinywa na mioyo.
Mwana mzuri Bwana Yesu, twakuomba tupeleke pale wakuimbiapo malaika nyimbo nzuri.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook