Wajibu Mwema Watoka Kwako
Lyrics kama ilivyo katika "Mwimbieni Bwana (Tumwabudu Mungu wetu)"
K: Wajibu mwema watoka kwako,
Bwana mwenye utukufu.
Neno jema ndilo Jina lako.

W: /: Yesu ni mwanzo wa kazi shambani,
tena ni Bwana, wa nguvu kwa utume wetu. :/
K: Watendakazi mwako shambani,
uwape matumaini.
Nazo nguvu wakiwa kazini.

W: /: Watende yote kwa uaminifu,
wawe makini, huduma isiharibike. :/
K:/ Wapate heri kuyasikia uliyoyaagiza.
Waje nao kutuhubiria.

W: /: Tena kazini wakaelezee Neno
Kwa wazi, na kweli ya uzima wako. :/
K: Wajihadhari wawe na hamu,
kushika na kufahamu.
Jina lako likawarehemu.

W: /: Ni wachungaji, wajue hilo tu
si watawala. Bwana ajifunue kwao. :/
K: Unawatuma katika kundi,
kwa bidii na juhudi.\Nasi kwao tuwe mashahidi.

W: /: Ushangiliwe kwa neema yako,
na kundi lako lijue lina viongozi. :/


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook