Mungu ni wa Utukufu
Lyrics kama ilivyo katika "Mwimbieni Bwana (Tumwabudu Mungu wetu)"
Mungu ni wa utukufu
panapo mbingu juu,
na kwao wampendezao
duniani raha kuu.
Sikieni inchi zote
huko mjini bethlehemu:
/: Kristo amezaliwa,
Bwana wetu daima. :/
Watu na malaika wote
wanamtukuza Yesu,
ashukaye toka Mbingu
kuwa kama maskini.
Akaacha enzi yake,
akavaa unyenyekevu:
/: Kristo amezaliwa,.:/
Asifiwe Mungu Mwana
na Mwokozi wa watu,
mleta mwanga na uzima
Yesu mshinda kuzimu,
Mfalme wa utengamano
huko njini Bethlehemu.
/: Kristo amezaliwa,..:/


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook