Jina lake Yesu Tamu
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Jina lake Yesu tamu; tukilisikia, hutupoza, tena hamu hutuondolea.
Roho iliyoumia, kwalo hutibika, chakula, njaani pia; raha, tukichoka.
Jina hili ni msingi, ngao, ngome, mwamba, kwa hili napata wingi, kwangu ni akiba.
Yesu, mchunga, rafiki, mwalimu, kuhani, mwanzo, mwisho, njia, haki, uzima kifoni.
Moyo wangu hauwezi, kukusifu kweli, ila sifa zangu hizi, Bwana zikubali.
Na utakaponiita, kuja kwako Bwana, huko kwako sitaacha, kukusifu sana.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook