Wimbi litakasalo
O Now I See The Crimson Wave
Nyimbo za Kristo ( #188 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Nyimbo za Kristo"
Wimbi la damu la Yesu linatutakasa
Aliumia kusudi tupate uzima
Wimbi la damu naona naingia natakaswa!
Bwana asifiwe sana hutakasa hutakasa
Damu inasema kwangu nasikia mvuto
Inasema mvuto moyo wangu hutakaswa nayo
Naondoka kutembea kwa nuru ya mbungu
Mavazi yamesafishwa moyoni ni Yesu
Neema ni ya ajabu kutakaswa ndani!
Na kuwa naye Yesu tu aliye mwokozi


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook