Yesu u Nyota Kubwa
Lyrics kama ilivyo katika "Mwimbieni Bwana (Tumwabudu Mungu wetu)"
Yesu, u nyota kubwa,
itaokayo kwa Yakobo,
moyo wangu wapenda
kukutumikia leo.
Ukubali vipaji
niviletavyo mimi.
Ninaleta dhahabu,
ndio kukutegemea,
nalo ni paji lako,
ulilonipa mwenyewe;
nikushike kwa kweli
hata majaribuni.
Nao uvumba wangu
ni maombi yangu mimi;
midomo na mioyo
isikome kuyatoa.
Uyakubali haya
kuwa uvumba mzuri.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook