Mle Kaburini, Yesu Mwokozi
Tenzi za rohoni ( #96 ) , Nyimbo standard ( #176 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Mle kaburini, Yesu Mwokozi! Alilazwa chini, Bwana wangu!
Bwana! Amefufuka, kifo kimeshindwa kabisa! Gizani mle alitoka chini, sasa atawala huko Mbinguni! Yu hai! Yu hai! Bwana Yesu yu hai!
Aungoja huo, Yesu Mwokozi! Mchana ujao, Bwana wangu!
Walinda kaburi, Yesu Mwokozi! Bure ni muhuri, Bwana wangu!
Kifo kimeshindwa, Yesu mwokozi! Pingu zimevunjwa, Bwana wangu!


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook