Huyo ndiye! Anashuka
Tenzi za rohoni ( #98 ) , Nyimbo standard ( #41 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Huyo ndiye! anaskuka, aliyetufilia, wengi waliookoka, wakimfurahia, Aleluya! Yesu aturudia.
Sote tutamtazama, amekaa kitini, nao waliomcoma, kumkaza mtini, Na kilio, wamuone enzini..
Alama za kifo chake, hata sasa anazo, na waaminifu wake, wapendezewa nazo. Alipata, Kwetu alama hizo.
Wokovu utakiwao, sasa wapatikana, na watakatifu hao, mbinguni wakutana. Kumlaki, ndiyo siku ya Bwana
Wakusujudie wote, mbele ya kiti chako. Zako, Bwana, nguvu zote itwae milki yako. Njoo Bwana, sisi tu watu wako.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook