Yesu akwita
Tenzi za rohoni ( #43 ) , Nyimbo standard ( #131 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Yesu akwita, chanena chuo: uje leo, uje leo; kwani kusita? Akwita, njoo; unatanga upeo.
Hwita leo, hwita leo. Yesu akwita kwa upole akwita leo.
Waliochoka, wapumzike, hwita leo, hwita leo: wenye mizigo, wakamtweke, wapate mapumuo.
Anakungoja, uliye yote, uje leo, uje leo; uliyekosa usijifiche: woshwe, uvikwe nguo.
Yesu asihi wakawiao, waje leo, waje leo. Watafurahi waaminio; usije kwani? Njoo.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook