Kazi yangu Ikiisha
Tenzi za rohoni ( #102 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka; na kuvaa kutokuharibika, nitamjua Mwokozi nifikapo ng'amboni; atakuwa wa kwanza kunilaki
Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso; Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.
Furaha nitapata nikiona makao, Bwana aliyotuandalia; nitamsifu mwokozi, kwa rehema na pendo, vilivyonipa pahali Mbinguni.
Nao waliokufa katika Bwana Yesu, nitawaona tena huko juu; lakini nifikapo kwake huko Mbinguni, nataka kumwona Mwokozi kwanza.
Milangoni mwa mji Bwana atanipitisha, pasipo machozi wala huzuni. Nitauimba wimbo wa milele; lakini nataka kumwona Mwokozi kwanza.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook