Faraja Tumaini Langu
Lyrics kama ilivyo katika "Mwimbieni Bwana (Tumwabudu Mungu wetu)"
Faraja, tumaini langu
usiniache gizani.
Moyo ni wazi kukungoja,
Ee Yesu uniingie.
Furaha ya mbingu na
nchi, Mwana adamu na
Mungu;
Ee nuru kutoka mbinguni,
Angaza moyo wangu huu.
Mtoto mpendwa,
nakuomba, chagua moyo
wangu huu, ufanye kuwa
hori lako ukalazwe humo
wewe.
Ili nipate mwisho mwema
wa shida yangu na vita.
Zaliwa ndani yangu Yesu,
na ndani yangu ukue.
Mwokozi wangu utulize,
tumaini hili kubwa.
Ukija nitakupokea
Kwa roho nyenyekevu,
hii.Uweza wangu wote
pia wakungojea kwa
uchu. nataka kukutumikia:
Njoo, Yesu usikawie


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook