Tuimbe na Kusifu
Lyrics kama ilivyo katika "Mwimbieni Bwana (Tumwabudu Mungu wetu)"
Tuimba na kusifu
kwa nyimbo za furaha:
Yesu Bwana wetu
amezaliwa leo
zizini Bethlehemu
Furaha ya mioyo.
Mponya na mwokozi,
tunakusifu.
Nakutamani sana,
Uliyetoka juu.
Ee mwokozi mwema
tuliza moyo wangu,
unipe neema yako,
Kitoto cha huruma.
Univute juu.
Rehema zake Mungu
ni nyingi, alimtuma
Mwana wake Yesu,
awakomboe watu,
atufanyie njia,
tufike tena kwetu.
Kwetu ni kwa Mungu,
kwetu kwa Mungu
Na watu wakaao
katika giza wote
wanakungojea
Wewe mwokozi wetu,
na kukufurahia
uliyetukomboa.
Yesu Bwana wetu
twakutukuza.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook