Bwana Mungu, nashangaa kabisa
How great thou art
Tenzi za rohoni ( #114 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Bwana Mungu, nashangaa kabisa, nikitazama kama vilivyo,
nyota, ngurumo, vitu vingi vyote, viumbwavyo kwa uwezo wako.
Roho yangu na ikuimbie, jinsi wewe ulivyo mkuu,
Roho yangu na ikuimbie, jinsi wewe ulivyo mkuu.
Nikitembea pote duniani, ndege huimba nawasikia,
milima hupendeza macho sana, upepo nao nafurahia.
Nikikumbuka kama wewe Mungu, ulivyompleleka mwanao,
afe azichukue dhambi zetu, kuyatambua ni vigumu mno.
Yesu mwokozi utakaporudi, kunichukua kwenda mbinguni,
nitashukuru na kwimba milele, wote wajue jinsi ulivyo.

Bwana Mungu, nashangaa kabisa -

Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook