Malkia Njooni Toka Juu
Lyrics kama ilivyo katika "Mwimbieni Bwana (Tumwabudu Mungu wetu)"
Kitoto mpenzi lala wee,
Kitoto wa Mbingu!
Malaika wakupepea
ulale kwa raha.
Nasi maskini wachunga
Tunakubembeleza wee.
Lala, ulale:
Kitoto wee, ulale.
Maria kwa upendo mkuu
amlaza vizuri.
Yosefu amekaa kimya
ili asimwamshe.
Na wanyama wa
nyumbani
wemenyamaza kabisa:
Lala, ulale:
Kitoto wee, ulale.
Yesu atakapokua,
watakuumiza
Kilimani pa golgota,
utasulibishwa.
Kwa hiyo sasa lala tu!
Kwa raha na utulivu!
Lala, ulale:
Kitoto wee, ulale.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook