Ni Salama rohoni mwangu
It is well with my soul
Tenzi za rohoni ( #23 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Nionapo amani kama shwari, ama nionapo shida;
Kwa mambo yote umenijulisha, ni salama rohoni mwangu.
Salama, rohoni, ni salama rohoni mwangu!
Ingawa shetani atanitesa, nitajipa moyo
kwani Kristo ameona unyonge wangu, amekufa kwa roho yangu.
Dhambi zangu zote, wala si nusu, zimewekwa msalabani;
Wala sichukui laana yake, ni salama rohoni mwangu.
Ee Bwana himiza siku ya kuja, panda itakapolia;
utakaposhuka sitaogopa, ni salama rohoni mwangu.

Ni Salama rohoni mwangu -

Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook