Peleleza Ndani yangu
Tenzi za rohoni ( #59 ) , Nyimbo standard ( #349 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Peleleza ndani yangu, iwe safi nia, kwangu kama kwako Mungu, Idhihiri pia.
Peleleza moyo wangu unifunulie, yaliyomo ndani yangu nami niyajue.
Kwanza washe zako tambi, kumefunga giza; Nijue ambavyo dhambi ni la kuchukiza.
Peleleza na mawazo ni mbegu za mambo, asili ya machukizo, maumbuo - umbo.
Zidi kuyapeleleza katikati yangu, hata wishe nifundisha udhaifu wangu.
Hapo nikikwinamia mbele zako, Mungu, hakika nitakujua, u mpenzi wangu.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook