Fungua Milango Yote
Lyrics kama ilivyo katika "Mwimbieni Bwana (Tumwabudu Mungu wetu)"
Fungua Milango yote,
yuaja Bwana wa mbinguni.
Mfalme wa wafalme wote,
Mwokozi wa ulimwengu.
atuletea uzima;
kwa hiyo tumwimbieni:
Tumsifu Mungu,
aliyetuumba.
Ni mwenye haki na shujaa,
Upole mwingi amevaa;
Rehema ni taji yake,
huruma ni fimbo yake:
Atuondolea shida.
Kwa hiyo tumwimbieni
Tumsifu Mungu,
Mwokozi wetu mkuu.
Miji na nchi huchipushwa,


afikako Mfalme huyu;


nayo mioyo huchekeshwa,


anayoingia Yesu.


Ndiye jua la furaha


linalotufurahisha.

Tumsifuni Mungu

mtunza mioyo yetu.
Fungua Milango yote! Tengenezeni mioyo! Makuti yawe upole, furaha, pendo, amani. Mwokozi atawajia, areta raha, uzima Tumsifuni Mungu, ni mwenye rehema.
Njoo, Mwokozi wangu Yesu, nakufungulia moyo. Uingie na rehema, nione upole wako. Uniongoze kwa roho, nifike kwako mbinguni. jina lako Bwana lisifiwe pote


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook