Roho yangu Hima
Tenzi za rohoni ( #21 ) , Nyimbo standard ( #407 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Roho yangu hima, na taa yako, kaiwashe vyema, hapa si pako; nguvu zote pia za duniani, hazitakudhuru ukiamini.
Yesu yuko mbele, Yesu yu nyuma, Yesu vivyo kando, walindwa vyema.
Adui shetani, na nguvu zake, Bwana ameshinda, kwa kifo chake; wewe nguvu huna, huna kabisa, ndiwe mpungufu, mnyonge hasa.
Toka na mapema, mbele ya wote, omba, bisha sana, maisha yote; vita vikaliko, macho ukae, jivike silaha, nawe sishindwe.
Bwana Yesu ndiye, kwako mchunga, neno lake Bwana, ndilo upanga; Mbingu zitakwisha, na nchi pia, neno lake Bwana laendelea.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook