Bwana uliyewaita
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Bwana uliyewaita watakatifu wako,
Wawe mitume, wachunga, walishe kundi lako;
wanyonge na wenye hofu wakawa mashujaa
, na wapole wa kunena wasiwe kunyamaa.
Hata leo wawataka watakatifu wako,
nawe wauliza tena ni nani aliyeko,
atakaye nimtume afundishe vijana?
"Ni tayari, Bwana wangu, nitume mimi Bwana."
Nitume na mimi Bwana kama ulivyotumwa,
habari ya msamaha na dhambi kutubiwa,
niwahubiri wakosa na waliopotea,
wokovu u wake Bwana aliyewafilia.
Astahiliye hapana kutamka habari,
lakini wewe waweza kutufanya tayari.
neno lako tulijue, tupe na roho yako,
hayatakuwa ya bure, haya maneno yako.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook