Baba, Mwana, Roho
Tenzi za rohoni ( #6 ) , Nyimbo standard ( #1 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Baba, Mwana Roho, Mungu mwenye enzi, kila tukiamka tunakuabudu. Baba, Mwana Roho, Mungu wa mapenzi, ewe utatu, tunakusifu.
Baba, Mwana, Roho, wakuaminio, wanakutolea shukrani zao. Wakusujudia malaika nao; wewe u mwanzo, nawe u mwisho.
Baba, Mwana, Roho, sisi tu gizani, utukufu wako hauoni kosa; U mtakatifu, nawe u mapenzi, U peke yako, mwenzio huna.
Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi, ulivyoviumba vyote vyakusifu: Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi, Ewe utatu, tunakusifu.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook