Anisikiaye Aliye Yote
Tenzi za rohoni ( #36 ) , Nyimbo standard ( #125 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Anisikiaye, aliye yote; sasa litangae, wajue wote, duniani kote neno wapate, atakaye na aje!
Ni "Atakaye", ni "atakaye", pwani hata bara, na litangae; ni Baba Mpenzi alinganaye atakaye na aje.
Anijiliaye, Yesu asema, asikawe, aje hima mapema; ndimi njia, kweli, ndimi uzima; atakaye na aje!
Atakaye aje, ndivyo ahadi; atakaye hiyo, haitarudi! atakaye lake, ni la ahadi! Atakaye na aje.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook