Safari
Tenzi za rohoni ( #65 ) , Nyimbo standard ( #389 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Katika safari yetu kwenda mbinguni, tusiishe siku zetu usingizini.
Ng'oani! Tujifungeni, twende zetu juu! Kristo ndiye kiongozi; tusihofu tu.
Atwekwe badala yetu, mwenyewe Bwana; Yesu kiongozi wetu atapokea.
Kisimani, maji tele, maji mazima! Maji hayo, ya milele yana neema.
Njiani miiba mingi, yatuumiza; Hofu na hatari nyingi, sana zakaza.
Kweli, njia ya mbinguni ni ya mashaka; Tuwe na Yesu njiani, mara hufika.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook