Watoto Njooni Bethlehemu
Lyrics kama ilivyo katika "Mwimbieni Bwana (Tumwabudu Mungu wetu)"
Watoto njooni,
Bethlehemu,
njooni zizini kuona
makuu
Mungu aliyotutendea leo,
watoto waone furaha
kubwa.
Twaona kitoto kizuri
hapa, wazee wamtazama,
wachungaji wote
wamwangukia
malaika wa mbingu
wanamwimbia.
Pigeni magoti na
wachungaji!
Wakubwa, wadogo
tumnyenyekee!
Tuimbe na sisi kwa
furaha kuu,nyimbo za
kumsifu Mwokozi Yesu!
Watoka mbinguni
utuokoe,
waona uchungu sababu
yetu,
Leo wazaliwa mwana
kikiwa.
Halafu wateswa, unatufia
Twapenda kukupa mioyo
yetu, twataka kukutumikia
vema.
Takasa mioyo ikupendeze,
tupate kufika kwako
mbinguni.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook