Mwamba wenye imara
Rock of ages
Tenzi za rohoni ( #58 ) , Nyimbo standard ( #106 ) , Nyimbo za Kristo ( #192 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Mwamba wenye imara, kwako nitajificha!
maji hayo na damu, yaliyotoka humu,
hunisafi na dhambi, hunifanya mshindi
Kwa kazi zote pia , sitimizi sheria.
nijapofanya bidii, nikilia nakudhii,
hayaishi makosa: Ndiwe wa kuokoa.
Sina cha mkononi, Naja Msalabani;
Nili tupu, nivike; Ni mnyonge, nishike;
Nili mchafu naja, Nioshe nisijafa.
Nikungojapo chini, nakwenda kaburini;
nipaapo Mbinguni, na kukwona enzini;
roho yangu na iwe rahani mwako wewe.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook