Nasikia Kuitwa
Tenzi za rohoni ( #40 ) , Nyimbo standard ( #252 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Nasikia kwitwa, na sauti yako, nikasafiwe kwa damu, ya kwangikwa kwako.
Nimesogea Mtini pako, unisafi kwa damu, ya kwangikwa kwako.
Ni mnuonge kweli, umenipa nguvu, ulivyonisafi taka, ni utimilivu.
Yesu hunijuvya; mapenzi, imani; Tumai, amani, radhi, hapa na Mbinguni.
Huipa imara, kazi yake, ndani; huongezeka neema, ashindwe Shetani.
Huishuhudia, Myoyo ya imani ya kuzipata ahadi, wakimuamini.
Napata wokovu, wema na neema; kwako Bwana nina nguvu, na haki daima.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook