Tazameni Huyo Ndiye
Tenzi za rohoni ( #97 ) , Nyimbo standard ( #186 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Tazameni huyo ndiye, mwenye kushinda vita; haya, tumsujudie; nyara anazileta; watu wote msifuni, sasa yumo kitini.
Msifuni malaika, mtukuzeni sana, wote waliookoka watamsifu Bwana; watu wote msifuni, sasa yumo kitini.
Walimfanya dhihaka zamani wenye shari, kwao waliookoka ni Bwana wa fahari; watu wote msifuni. sasa yumo kitini.
Nyimbo nzuri, sikizeni, ni nyimbo za sifa kuu, za Bwana Yesu kitini, kutawazwa, yeye tu; watu wote msifuni, sasa yumo kitini.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook