Twonane Milele
Tenzi za rohoni ( #101 ) , Nyimbo standard ( #192 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Nyimbo na tuziimbe tena, za alivyotupenda mbele; kwa damu ya thamani sana! Mbinguni twonane milele.
Twonane milele, twonane bandarini kule; Twonane milele, twonane bandarini kule.
Hupozwa kila aoshwaye, kwa damu ya Kondoo yule; ataishi afurahiye, vya Yesu mbinguni milele.
Hata sasa hufurahia, tamu yake mapenzi yale, je, kwake tukifikilia, kutofarakana milele?
Twende mbele kwa jina lake, hata aje mwokozi yule, atatukaribisha kwake, tutawale naye milele.
Sauti zetu tuinue, kumsifu mwokozi, ili watu wote wajue, wokovu u kwake milele.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook