Jina la Yesu, salamu!
Tenzi za rohoni ( #4 ) , Nyimbo standard ( #507 ) , Nyimbo za Imani yetu ( #11 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Jina la Yesu salamu! lisujudieni, lisujudieni,
ninyi mbinguni, hukumu na enzi mpeni
Enzi na apewe kwetu, watetea dini;
mtukuzeni Bwana wenu, na enzi mpeni.
Enyi mbegu ya rehema, Nanyi msifuni;
Mmeponywa kwa neema, Na enzi mpeni.
Wenye dhambi kumbukeni ya msalabani,
Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni.
Kila mtu duniani Msujudieni,
Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni.
Sisi na wao pamoja Tu mumo sifani,
Milele sifa ni moja, Ni "Enzi mpeni."


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook