Ewe Roho wa Mbinguni
Tenzi za rohoni ( #12 ) , Nyimbo standard ( #210 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Ewe roho wa Mbinguni, Uje kwetu sasa. Ufanye makazi yako, ndani ya kanisa.
Ndiwe mwanga, umulike, tupate jikana; mengi kwetu yapunguka, tujaze, Bwana.
Ndiwe moto, teketeza taka zetu zote; Moyo na iwe sadaka, ya Mwokozi, yote.
Ndiwe umande, na kwako tutaburudika, nchi kavu itakuwa, ni yenye baraka.
Roho wa Mbinguni, uwe nasi hapa chini, mwili uufananishe, na kichwa Mbinguni.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook