Ni "Mtu wa Simanzi"
Tenzi za rohoni ( #85 ) , Nyimbo standard ( #160 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Ni "Mtu wa Simanzi", mwana wa mwenye enzi, mwenye mengi mapenzi! Asifiwe Bwana Yesu!
Akawa matesoni, "Mungu mwana| yakini akatoka Mbinguni: Asifiwe Bwana Yesu!
Akapata dhihaka, mzoea - mashaka, ndiye yetu sadaka: Asifiwe Bwana Yesu!
Tu wenye dhambi sana; kwake dhambi hamna, na Mungu twapatana: Asifiwe Bwana Yesu!
Alikufa mtini, akalia dhikini, sasa yuko Mbinguni: Asifiwe Bwana Yesu!
Punde atarejea, Yesu kutunyakua, ndipo tutamwimbia: Asifiwe Bwana Yesu!


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook