Juu yake langu Shaka
Tenzi za rohoni ( #134 ) , Nyimbo standard ( #299 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Juu yake langu shaka Yesu namuwekea, nami sitafedheheka, nikimtegemea.
Natumai, natumai, natumai kwake tu; Natumai, natumai, natumai kwake tu.
Juu yake, dhambi zangu; aniosha kwa damu; nionekane kwa Mungu, nisiye na laumu.
Juu yake yangu hofu; kwake nimetulia; sipotei kwa upofu, njia aning'azia.
Juu yake raha yangu; humuangalia tu; mwenye kila ulimwengu, aniruzuku na huu.
Juu yake, moyo wangu; hali yangu na mali; Mimi wake, Yeye wangu, twapasana kamili.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook