Damu Imebubujika
There is a fountain filled with Blood
Tenzi za rohoni ( #86 ) , Nyimbo standard ( #145 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Damu imebubujika,
ni ya Imanweli,
wakioga wenye taka,
husafiwa kweli.
Ilimpa kushukuru,
Mwivi mautini;
Nami nisiye udhuru,
yanisafi ndani.
Kondoo wa kuuawa,
damu ina nguvu,
wako wote kuokoa,
kwa utimilivu.
Bwana tangu damu yako,
kunisafi kale,
nimeimba sifa zako;
Taimba milele.
Nikifa tazidi kwimba,
sifa za wokovu,
ulimi ujaponyamaa,
vumbini mwa ufu.
Bwana, umenikirimu,
nisiyestahili,
kwa damu yako, sehemu,
ya mali ya kweli.
Nikubali kukwimbia,
Mbinguni milele,
Mungu nitakusifia,
jina lako pweke.

Damu Imebubujika -

Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook