Nataka Nimjue Yesu
More About Jesus
Tenzi za rohoni ( #92 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Nataka nimjue Yesu, na nizidi kumfahamu,
nijue pendo lake, na wokovu wake kamili.
Zaidi, zaidi, nimfahamu Yesu,
nijue pendo lake, na wokovu wake kamili.
Nataka nione Yesu, na nizidi kusikia,
anenapo kitabuni, kujidhihirisha kwangu.
Nataka nifahamu, na nizidi kupambanua, mapenzi yake,
nifanye yale yanayompendeza.
Nataka nikae naye, kwa mazungumzo zaidi,
nizidi kuwaonyesha, wengine wokovu wake.

Nataka Nimjue Yesu -

Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook