Twamsifu Mungu
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Twamsifu Mungu, kwa mwana wa Pendo, Aliyetufilia na kupaa juu.
Aleluya! Usifiwe; Aleluya! Amin. Aleluya! Usifiwe, utubariki.
Twamsifu Mungu, kwa Roho Mtukufu, ametufunulia Mwokozi wetu.
Twamsifu mwana, aliyetufia, aliyetwaa dhambi akazifuta.
Twamsifu Mungu, wa neema yote, ametukomboa akatuongoza.
Tuamshe tena, tujaze na pendo, na moyoni uwashe moto wa Roho.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook