Mmoja Ndiye Tumpendaye
Lyrics kama ilivyo katika "Mwimbieni Bwana (Tumwabudu Mungu wetu)"
Mmoja ndiye
tumpendaye,
aliyetoa mwili wake
akikubali mateso.
Twakupa mioyo yetu
Mwokozi uliyetufia,
twapenda kuwa wako tu.
Bwana tukubali!
Ututengeneze sisi wako.
Nuru yako itung'aze
tusipotee gizani.
Sisi hatukukuita,
ila umetuita wewe,
huruma yako ni kubwa.
Nguvu zetu hazitoshi,
kukuanyia kazi njema
usipotutia nguvu.
Shida yetu sisi
ndio ulegevu, uondoe;
nia zetu zigeuzwe
tufanye kazi kwa bidii.
Yesu, wewe umesema:
"Watenda kazi ni wachache
kwenye mavuno ya Bwana"
Twaimba: Tutume na sisi,
tualike wageni wengi,
nyumba ya Bwana ijae.
Heri watu wale
uliochagua kuja kwako
kwenye raha na furaha,
milele hata milele.
Uwahurumie watu walio mbali na wokovu wanaoshikwa na giza. Hawajasikia bado utume mwema wa wokovu tunaopewa na Mungu. Jua la uzima liche hata kwako. Njoo Mwokozi! Tangilia! Twafuata, Ukifungua milango.
Tunataka kutangaza
habari ya upendo wako,
ya moyo wako wa kweli.
Tutawaonyesha watu
msalaba wako siku zote,
mpaka washindwe
mioyoni.
Kwani Neno lako
lina nguvu kubwa
ya kushinda.
mzigo wako ni mwepesi.
mlango wa mbingu ni
wazo.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook