Tutakaa Mahali Pa Maji
We’ll Tarry by the Living Waters
Nyimbo za Kristo ( #181 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Nyimbo za Kristo"
Mahali pa maji mazuri maji ya uzima;
Anapotungoja Yesu tutakaribishwa.
Mahali pa maji mazuri, penye maji ya uzima;
Tutakaa na Mwokozi, chemchemi ya uzima.
Tunapochoka safarini, tamu kupumzika.
Panapo maji ya uzima yatufurahisha.
Una kiu? Uje kwa Yesu, utaburudishwa;
Yesu yu maji ya uzima, unywe,uokoke.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook