Nimekombolewa na Yesu
Redeemed! How O Love to Proclaim It
Tenzi za rohoni ( #25 ) , Nyimbo za Kristo ( #35 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Nimekombolewa na Yesu, aliyenirehemia ( na sasa nimefurahi );
kwa bei ya mauti yake nimekuwa mtoto wake.
Kombolewa! Nakombolewa na damu;
kombolewa! mimi mwana wake kweli.
Kukombolewa nafurahi, kupita lugha kutamka;
kulionyesha pendo lake, nimekuwa mtoto wake.
Nitamwona uzuri wake, mfalme wangu wa ajabu;
na sasa najifurahisha, katika neema yake.
Najua taji imewekwa, Mbinguni tayari kwangu;
muda kitambo atakuja, ili alipo, niwepo.

Nimekombolewa na Yesu -

Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook