Twenenda Sayuni
Tenzi za rohoni ( #108 ) , Nyimbo standard ( #514 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Mpendao Bwana ije raha yenu! Imbeni nyimbo za raha wa ibada yenu.
Twenenda Sayuni, mji mzuri Sayuni; twenenda juu Sayuni, ni maskani ya Mungu.
Wasiimbe wao wasioamini, watoto wa Mungu ndio waimbao chini.
Twaona rohoni baraka za Mungu, tusijafika Mbinguni kwenye utukufu.
Tutakapomwona, masumbuko basi, huwa maji ya uzima, anasa halisi.
Tupaaze sauti, na fute machozi, twenenda kwa Imanweli, naye ni Mwokozi.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook