Ni tabibu wa karibu
Great physician
Tenzi za rohoni ( #7 ) , Nyimbo standard ( #256 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Tenzi za rohoni"
Ni tabibu wa karibu; tabibu wa ajabu;
na rehema za daima; ni dawa yake njema.
Imbeni, malaika, sifa za Yesu Bwana;
pweke limetukuka jina lake Yesu.
Hatufai kuwa hai, wala hatutumai,
ila yeye kweli ndiye atupumzishaye.
Dhambi pia na hatia ametuchukulia;
Twenendeni na amani hata kwake mbinguni.
Huliona tamu jina, la Yesu kristo Bwana,
yuna sifa mwenye kufa asishindwe na kufa.
Kila mume asimame, sifa zake zivume;
Wanawake na washike kusifu jina lake.
Na vijana wote tena, wampendao sana,
waje kwake wawe wake kwa utumishi wake.

Ni tabibu wa karibu -

Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook