Msingi Wa Kanisa
Nyimbo za Kristo ( #195 ) ,
Lyrics kama ilivyo katika "Nyimbo za Kristo"
Msingi wa Kanisa Ndiye Yesu Bwana; Kiumbe chake kipya Akipenda sana;
Kutaka ‘kitafuta Alishuka chini, Naye kwa haja yake, Akafa Mtini.
Lina kila kabila Kisha ndiyo moja Wokovu wake una Mwokozi ndiyo moja;
Uzazi ni umoja. Moja tumaini. Chakula ni kimoja. Moja tumaini.
Watu hustaajabu Kwa mashaka yote. Yaipatayo nje Hata ndani mwote;
Ila watakatifu Humwomba, wakikesha Usiku ni kilio. Asubuhi raha.
Mashaka na taabu Hata vita vyake. Vyangoja matimizo Ya amani yake.
Ndipo kwa macho yetu Twone utukufu Kanisa ya kushinda itastarehe juu.


Like Tenzi Za Rohoni page on Facebook